Mkuu
wa Wilaya ya Moshi Mjini Dr Msengia akiaga baada ya kuitembelea timu
Serengeti Fiesta 2012 Mkoa wa Kilimanjaro jioni ya leo. Katikati ni
Erick Kussaga ambae ni Mzalishaji wa timu ya Fiesta mkoani humo.
Mkuu
wa Wilaya ya Moshi Mjini Mheshimiwa Dr Msengi akiwa na Afisa Uhusiano
wa Clouds Entertainment Co. LTD kwa upande wa Viongozi wa Taasisi za
Serikali na Vyama vya Siasa Ndugu Simalenga Simon wakati Mkuu huyo wa
Wilaya alipoitembelea timu ya amsha amsha ya tamasha la Serengeti
Fiesta 2012 Mkoani Kilimanjaro jioni hii.Tamasha la Serengeti Fiesta
2012 linatarajia kuzinduliwa rasmi kesho katika uwanja wa chuo cha
Ushiriki mkoani humo,ambapo msanii nyota kutoka nchini Kenya,CMB Prezoo
ataliongoza jahazi la wasanii mbalimbali kutoka hapa nyumbani,katika
tamasha hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni shilingi 5000 kwa kila
kichwa.
Mmoja
wa washabiki wa tamasha la Serengeti Fiesta damu akiwa na fulana yake
ya tamasha hilo lililowahi kufanyika mjini moshi lililopachikwa jina la
jipanguze kama uonavyo pichani.Wanaharakati anuai wa tamasha la
serengeti fiesta 2012 leo wameamsha amsha wakazi wa mji huo katika
maeneo mbalimbali ikiwemo Himo,Stendi kuu ya mabasi pamoja na soko la
Mbuyuni na kutoa zawadi ya mafuta ya gari/pikipiki na bajaji kutoka
kampuni ya Gapco ambayo ni sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo,kwa watu
kadhaa ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za awali ya tamasha lenyewe.
No comments